Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
020

Ta Ha 20:47 فاتياه فقولا انا رسولا ربك فارسل معنا بني اسراييل ولا تعذبهم قد جيناك باية من ربك والسلام على من اتبع الهدى ٤٧

20:47
فَأۡتِيَاهُ
فَقُولَآ
إِنَّا
رَسُولَا
رَبِّكَ
فَأَرۡسِلۡ
مَعَنَا
بَنِيٓ
إِسۡرَٰٓءِيلَ
وَلَا
تُعَذِّبۡهُمۡۖ
قَدۡ
جِئۡنَٰكَ
بِـَٔايَةٖ
مِّن
رَّبِّكَۖ
وَٱلسَّلَٰمُ
عَلَىٰ
مَنِ
ٱتَّبَعَ
ٱلۡهُدَىٰٓ
٤٧
Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Basi endeni kwake na mumwambie, ‘Sisi ni wajumbe wawili kutoka kwa Mola wako kwamba uwaache Wana wa Isrāīl na usiwakalifishe matendo wasiyoyaweza. Kwa hakika tumekujilia na ushahidi wa kimiujiza kutoka kwa Mola wako wenye kuonesha ukweli wetu katika ulinganizi wetu. Na kusalimika na adhabu ya Mwenye…
Basi endeni kwake na mumwambie, ‘Sisi ni wajumbe wawili kutoka kwa Mola wako kwamba uwaache Wana wa Isrāīl na usiwakalifishe matendo wasiyoyaweza. Kwa…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 20, Ukurasa 314, Juzuu 16

25. (Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu, 26. Na unifanyie nyepesi kazi yangu, 27. Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, 28. Wapate kufahamu maneno yangu. 29. Na nipe waziri katika watu wangu, 30. Harun, ndugu yangu. 31. Kwake yeye niongeze nguvu zangu. 32. Na umshirikishe katika kazi yangu. 33. Ili tukutakase sana. 34. Na tukukumbuke sana. 35. Hakika Wewe unatuona. 36. Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa! 37. Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine 38. Pale tulipo mfunulia mama yako yaliyo funuliwa, 39. Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo tokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu. 40. Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Musa! 41. Na nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu. 42. Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka. 43. Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. 44. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa. 45. Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri. 46. Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona. 47. Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu. 48. Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anaye kadhibisha na akapuuza.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia